🗓️ Ijumaa 20 Septemba, 2024.
📍 Kibondo, Kigoma.
Jimbo la Muhambwe limepokea Mwenge wa Uhuru kutoka Halmashauri ya Kasulu Vijijini Leo katika Uwanja wa Shule ya Msingi Busunzu 'B' ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa mbio za Mwenge wa Uhuru zinazoendelea nchini.
Katika Jimbo la Muhambwe, Mwenge wa Uhuru umezindua Miradi ya Maji, Madarasa, Bweni na Miundombinu mingine, Ufugaji wa Nyuki/ Utunzaji wa Mazingira, Kikundi Cha Vijana Wajasiriamali, Klabu ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa - Shule ya Msingi Nengo (Watoto wenye Uhitaji Maalumu) na kadhalika. Miradi yote imekaguliwa kikamilifu.
Akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Kibondo (Jimbo la Muhambwe), Ndg. Makwaya Joseph Makwaya Kwa niaba ya Kiongozi wa Msafara wa Mbio za Mwenge amewataka Wananchi wa Wilaya ya Kibondo kusimama Imara katika Utunzaji wa Mazingira, Kutunza Miundombinu ya Kijamii, Kulinda Afya, Kudumisha amani ya Taifa letu pamoja na kushiriki kikamilifu katika mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ifikapo 27 Novemba, 2024.
Aidha, Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Dkt. Florence George Samizi ameitaka jamii ya Wana-Muhambwe kuendelea kudumisha amani, Upendo na mshikamano katika Kulinda Maendeleo Makubwa yanayofanyika katika Jimbo yanayochagizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mkesha wa Mwenge wa Uhuru umefanyika katika viwanja vya Jumba la Maendeleo (Vijana) - Kibondo Mjini.
Imetolewa na:
Ofisi ya Mbunge,
Jimbo la Muhambwe.
0 Comments