TASAC YAKABIDHIWA BOTI YA DORIA (PB SAILBOAT),

 



Katibu Mkuu ofisi ya waziri mkuu(sera,bunge na uratibu),Dkt Jimmy Yonazi leo amekabidhi boti ya maalum ya doria (Pb Sailfish) kwa shirika la uwakala wa meli Tanzania (Tasac)ikiwa ni juhudi za serikali katika shughuli za usimamizi na usalama wa bahari

Akizungumza katika hafla fupi ya ukabidhianaji wa boti hiyo iliyofanyika katika chuo cha bahari (DMI)Jijini Dar Es Salaam leo Septemba 19,2024 Dkt Yonaz amesema Lengo kuu la kununuliwa kwa boti hiyo ni kuimarisha doria ili kukabiliana na vitendo vya kihalifu katika Bahari na Maziwa Makuu nchini.

Amesema doria hizo ni mwendelezo wa juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kukabialiana na vitendo vya kihalifu kama vile uvuvi haramu, uhamiaji haramu, usafirishaji wa dawa za kulevya, biashara za magendo na utoroshwaji wa nyara za Serikali.

" Boti hii kama ilivyoelezwa hapo awali, ilinunuliwa kupitia mradi wa Kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Bahari na Maziwa Makuu Nchini kwa ufadili wa Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP). Nitumie nafasi kuwashukuru sana wafadhili wetu hao kwa ufadhili wao na ushirikiano mkubwa waliotupatia wakati wote wa ununuzi wa boti hii"amesema Dkt Yonaz

Aidha Dkt Yonazi amesema ana imani  kuwa boti hii itatimiza lengo hilo na kuimarisha juhudi za Serikali za kukabiliana na vitendo vya kihalifu katika eneo la bahari huku akiitaka Tasac kuhakikisha boti hiyo inatunzwa vyema ma ikiwa ni pamoja na kufanya  shughuli ambazo ndiyo lengo la ununuzi wake na zile ambazo zitajitokeza huku  akisisitizia kuwa matumizi ya boti hiyo pia yazingatie Mwongozo wa Kitaifa wa Kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Bahari na Maziwa Makuu wa mwaka 2022.  

"Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu ina imani kubwa na uwezo wa TASAC katika usimamizi, uendeshaji na utunzaji wa boti hii. Hiyo ndiyo sababu iliyopelekea boti hii kukabidhiwa kwa Shirika hili. Ni imani yetu kuwa mtaitunza vizuri boti hii ikiwa ni pamoja na kuifanyia matengenezo kinga kwa wakati na hivyo kuwaongezea ufanisi katika kazi zenu za kila siku hususani katika ukaguzi kwa meli zinazoingia kwenye maji yetu ya ndani" amesema

Hata hivyo ameisisitiza Tasac kuendelea kufanya kazi kwa karibu na Idara ya Menejimenti ya Maafa iliyopo Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya kuweza kuratibu programu za uokozi kwa majanga ya majini na usalama wa bahari kwa ujumla. 


Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa shirika la uwakala wa meli Tanzania (TASAC) Mohamed Malick Salum ameishukuru serikali kupitia ofisi ya waziri Mkuu Kwa boti hiyo na kusema kuwa itakuwa na tija katika kupambàna na uhalifu wa bahari na ulinzi wa rasilimali za bahari.

Amesema TASAC ilishirikiana vyema na wataalamu wa  ofisi ya waziri Mkuu katika usanifu wa boti hiyo ambayo itachagiza shughuli za usalama wa bahari na maziwa makuu hapa nchini.

"Sisi Kama Tasac tutahakikisha boti hii inatunzwa vyema Kwa kushirikiana na vyombo vingine ikiwemo tume ya kupambàna na kidhibiti dawa za kulevya nchini (DCEA)pamoja na jeshi la wanamaji na taasisi nyinginezo Kwa hiyo Kwa boti hii ulinzi wa bahari,maziwa makuu na rasilimali zake Sasa ni wa uhakika"amesema 

Awali akizungumza katika hafla hiyo,Naibu katibu Mkuu wizara ya uchukuzi Nahodha Ludovick Nduhiye amesema kama wizara wataendelea kushirikiana na Tasac ili kuhakikisha boti hiyo inakuwa na msaada mkubwa Kwa Taifa,huku akisisitiza utunzaji madhubuti wa boti hiyo.







Post a Comment

0 Comments