Na mwandishi wetu
Katika ardhi yenye historia ya mashujaa wa maendeleo, Ndg. Ally Hapi(MNEC) Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi Taifa amefika mkoani Kagera kama radi inayong'ara katika anga la siasa, akileta ujumbe wa mshikamano, matumaini, na hatua thabiti kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa sawa sawa na Chama Cha Mapinduzi kinavo jipambanua.
Mapokezi yake hayakuwa ya kawaida; yalikuwa ni kama msafara wa ushindi unaoweka alama ya uthabiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Ukubwa wa Chama cha Mapinduzi.
"Kagera inahitaji siasa za hoja, si kelele za lawama!" Hivyo ndivyo alivyoanika maono ya Chama cha Mapinduzi mbele ya wanachama na wananchi.
Akisisitiza kuwa maendeleo yanahitaji vitendo, sio porojo kama Vyama vingine vinavyo leta, akiwataka viongozi wa vyama vya siasa kuacha lawama zisizo na tija na badala yake kuelekeza nguvu zao kwa wananchi kupitia ajenda za maendeleo na mikakati thabiti.
Zaidi alihimiza mshikamano ndani ya CCM huku akiwataka viongozi kuwa mfano wa maadili, heshima, na ufanisi katika kampeni zinazokuja. "Ushindi wa kweli haujengwi kwa maneno matupu, bali kwa mshikamano wa dhati na nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi!"
#UshindiWetuNiKuraYetu
#UchaguziSerikaliZaMitaa
#MaendeleoKwaVitendo
0 Comments