Na mwandishi wetu
Mbunge wa Viti Maalum Vijana Tanzania, Mhe. Juliana Didas Masaburi akihutubia mkutano wa hadhara amewaambia wananchi kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanya kazi kubwa hivyo kukifanya Chama Cha Mapinduzi kuendelea kuaminiwa kupewa dhamana ya wananchi kuongoza Serikali
Mbunge Masaburi amefanya Mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kibosho, Kata ya Kisutu Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani na ameendelea kuwanadi na kuwaombea kura za kishindo Wagombea wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Unaotarajiwa Kufanyika tarehe 27 Novemba, 2024.
"Serikali imejenga Vituo vya Afya 367 na Majengo ya Zahanati 980. Imefikisha Umeme Vijijini kwa asilimia 96.37% hivyo kufanya Vijiji 11,837 kati ya Vijiji 12,318 kupata huduma ya umeme. Zimejengwa Shule mpya za Msingi na Sekondari 3,631 na jumla ya Madarasa mapya 21,912" Amesema Juliana Didas Masaburi, Mbunge wa Viti Maalum Vijana Tanzania
Vilevile, Juliana Masaburi amezindua Shina la Njia Panda ya Vikawe, Kata ya Mapinga la Umoja wa Vijana wa CCM ambalo amelizindua rasmi tarehe 23.11.2024.
0 Comments