MBUNGE KAMANI AZINDUA PROGRAMU YA ELIMU, BIASHARA NA UTALII (EBU) JIJINI MWANZA

 




Na mwandishi wetu


Mbunge wa Vijana Taifa Mhe Ng'wasi Kamani ameshiriki kama Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Programu ya Elimu, Biashara na Utalii (EBU) iliyo ratibiwa na Msanii kutoka kiwanda cha filamu Tanzania Bi Rose Donatus Ndauka, iliyofanyika Novemba 23, 2024 Wag hill, luchelele jijini Mwanza.

Programu hii imeweza kuhudhuriwa na washiriki mbalimbali wakiwemo Vijana wafanyabiashara na wajasiriamali, wadau wa Maendeleo, wataalam wa masuala ya fedha na uchumi, fursa, uwekezaji na Masoko ambao walipata fursa ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uwekezaji katika Sekta ya Elimu, Biashara na Utalii.

Katika hafla hiyo, Mhe Ng'wasi Kamani (Mb) amewepongeza waratibu wa programu hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wao Bi Rose Ndauka kwa kuweza kukutanisha vijana kutoka maeneo tofauti, jambo ambalo lina tija katika safari ya kuwakwamua Vijana hao kiuchumi na kuhakikisha wanapata mafunzo na kujenga mahusiano mapya na vikundi tofauti vyenye uzoefu na vilivyofanikiwa ili kuwa na utamaduni wa kushikana mikono kwenye safari ya mafanikio bila kuwaacha wengine nyuma. 

Vilevile, ametumia jukwaa ilo kutoa wito kwa washiriki wa mafunzo hayo kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba, 2024. 

Amesema, Serikali imeweka mazingira rafiki na kuhakikisha kuwa kila raia anapata haki yake ya kupiga kura kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na wenyeviti wa vitongoji za mwaka 2024. 

Amesema, ni haki ya msingi ya kila mwananchi kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika kuamua nani atakayewaongoza kwenye ngazi za serikali za mitaa.

Amewataka watumie ushawishi walionao kwa jami kuwahamasisha wananchi kutumia haki yao ya kikatiba katika kujitokeza na kushiriki kuchagua viongozi wao.







Post a Comment

0 Comments