MBUNGE MAVUNDE AAHIDI KUSHIRIKIANA NA WAISLAMU MAJENGO KUKAMILISHA UJENZI WA MSIKITI

 



▪️Achangia saruji tani 10


▪️Awapongeza waumini kwa kujitolea ujenzi wa msikiti


▪️Aahidi kutafuta wadau wa kukamilisha ujenzi


📍Dodoma


Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amewaahidi waumini wa Msikiti wa Ghazal Masjid Majengo Jijini Dodoma kushirikiana nao bega kwa bega katika ukamilishaji wa msikiti huo uliopo eneo la Majengo.

Mavunde kayasema hayo leo Jijini Dodoma wakati wa Swala ya Ijumaa iliyofanyika Masjid Ghazal-Majengo  Dodoma.

“Nimefurahi sana kuona hatua kubwa ambayo ujenzi umefikia tangu tulipoanzisha zoezi la uchangishaji ujenzi nikiwa sehemu ya kamati ya ujenzi.

Waumini mmejitoa kwelikweli kumjengea Mwenyezi Mungu nyumba yake.

Naahidi kuendelea kuwapa ushirikiano kwa kutafuta wadau wengi zaidi ili tukamilishe ujenzi wa msikiti huu pamoja na kwamba nilichangia awali lakini pia nakabidhi kwenu saruji tani 10 isaidie kukamilisha ujenzi“Alisema Mavunde

Naye Sheikh wa Msikiti wa Ghazal Masjid,Sheikh Abdallah Athuman amemshukuru Mh. Mavunde kwa kuwa bega kwa bega na msikiti na kusimamia vyema utekelezaji wa wazo la kuanzisha ujenzi wa msikiti akiwa ni sehemu ya kamati ya ujenzi.

Awamu ya kwanza ya ukamilishaji wa msikiti huo kwa sasa unahitaji zaidi ya Shilingi 250 milioni.







Post a Comment

0 Comments