MBUNGE WA VITI MAALUM NKUPA AFANYA ZIARA KATIKA VITUO VYA WATU WENYE ULEMAVU

 




Mbunge wa Viti Maalum, anayewakilisha watu wenye ulemavu Tanzania, Mh.Stella Ikupa, amefanya ziara katika vituo vya watu wenye ulemavu, wasafirishaji abiria kupitia bajaji ndogo na kubwa, katika Jiji la Dar es Salaam.

Vituo alivyotembelea Mbunge Stella ni  Nyahaja Uhasibu Group kilichopo pembezoni mwa Chuo Cha Uhasibu TIA, Temeke, Kituo cha Ocean Road cha bajaji ndogo cha wanawake, kituo cha bajaji kubwa na ndogo cha feli cha wanaume,(WABADA) kituo cha wanaume cha Mnazi Mmoja WABAKUTA.

Akizungumza katika vituo hivyo, Mbunge Mh.Stella Ikupa, aliwapongeza wasafirishaji hao wa abiria wenye ulemavu kwa Udhubutu wao mkubwa wa kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kupitia shughuli zao.

 Mbunge Stella, aliwasisitiza wasafirishaji hao wa abiria wenye ulemavu, kuendelea kuiunga mkono serikali ya Rais Dkt.Samia  kwa kujitokeza kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

 Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliyoko mbele yetu, unaotarajiwa kufanyika Jumatano Novemba 27, kwani ni haki ya kila mwananchi kumchagua kiongozi anayemtaka.

Amesema, serikali ya Rais Dkt. Samia haijawasahau  watu wenye ulemavu, kwani imeendelea kutoa mikopo ya asilimia kumi isiyo na riba ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa walemavu na kuwasaidia kukuza uchumi wao.

Mbunge ikupa amesema serikali ya Rais Dk.samia imeweka mazingira wezeshi kwa walemavu kufanya shughuli zao, ikiwemo kuruhusiwa kufanya shughuli zao katikati ya maji hususan Jiji la Dar es Salaam jambo ambalo limeendelea kuleta tija kubwa kwao.

Katika hatua nyingine, Mh.Mbunge Stella, alisikiliza changamoto mbalimbali za walemavu huku zingine akizitolea ufafanuzi ikiwemo Ile ya mikopo ya asilimia 10 isiyo na riba.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Makada wa CCM Taifa, Pili Birahi alimpongeza Mbunge Stella kwa ziara hiyo muhimu ya kuwafikia watu wenye ulemavu jambo ambalo limekuwa faraja kubwa kwao.

Mwenyekiti wa Kikundi cha Nyahaja Uhasibu Group, alimshukuru Mbunge Stella huku akiahidi kumuunga mkono kwa kuhakikisha anawahamasisha wajumbe na watu wengine ulemavu kupiga kura.

Naye, Diwani wa Kata ya Kivukoni, Shariki Choughule alisema wamefurahishwa na ziara ya Mbunge Ikupa kukutana na watu wenye ulemavu kata yake, huku akiwasisitiza kuwachagua viongozi wa CCM, ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais Dk.samia kwa kutoa fedha nyingi za maendeleo .

Vilevile, Mwenyekiti wa Madereva wa bajaji za watu wenye ulemavu Tanzania -WABAKUTA, Mathew Kasiririka alisema wako tayari kuiunga mkono serikali ya Rais Samia kuwachagua viongozi wa CCM katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwani imewapa uhuru wa kufanya shughuli zao kwa amani.






Post a Comment

0 Comments