Na mwandishi wetu
Mhe. Santiel Eric Kirumba, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, tarehe 20 Novemba, 2024 amezindua rasmi kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024
Mbunge Santiel ameshiriki na kuzindua kampeni kwa kufanya mkutano wa hadhara katika wa Kata Nyasubi huku akiwanadi wagombea wa CCM wa Mitaa Mitatu wanaogombea kuwania nafasi za uongozi huku wakiahidi kuwatumikia wananchi pindi watakapochaguliwa.
"Ushindi ni lazima kwa CCM kwani Ilani ya uchaguzi ya CCM imetekelezwa vyema. CCM tunasonga mbele katika Safari ya kuelekea tarehe 27/11/2024. Wananchi msiache kwenda kupiga kura ili tuendelee kupanga maendeleo kwa pamoja" - Mhe. Santiel Kirumba
0 Comments