WAZIRI MASAUNI ASISITIZA NYUMBA ZA IBADA ZITUMIKE KUHAMASISHA AMANI

 





Na Mwandishi Wetu- MoHA, Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesisitiza watanzania kuendelea kudumisha amani sambamba na kutumia nyumba za ibada  kuhamasisha na kutoa mafundisho ya dini yatakayo dumisha amani.

Waziri Masauni amesema hayo leo Novemba 29, 2024 wakati akifungua Msikiti wa Tawhid eneo la Coco Beach ( Zamani Msikiti wa Makuti) ambapo amesema "Tanzania ni Nchi ambayo tunavumiliana sana na ndio maana ni rahisi kukuta watu wenye dini tofauti wanaishi kwa upendo, mshikamano bila kubaguana wala kuchukiana".

Hata hivyo Waziri Masauni amesema utamaduni wa kuvumiliana umejengewa misingi imara na waasisi wa taifa letu " ndio maana unaweza kukuta nyumba ya ibada ya dini moja anatokea muumini wa dini nyingine kutoa mchango wa ujenzi ni suala linalofanya nchi yetu kuzidi kuwa na amani" alisema Waziri Masauni.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya The Islamic Foundation,  Aref Nahd amesema kukamilika kwa msikiti huo utasaidia waumini kutekeleza ibada ya swala tano kwa waislam wanaokwenda kwenye fukwe hizo kutembea na kupumzika.

Aidha Ufunguzi huo pia umehudhuriwa na  Balozi wa Qatar nchini, Mhe. Fahad Rashid Al Marekhi, Balozi wa Uturuki nchini, Dkt. Mehment Gulluoglu, Masheikh na waumini wa dini ya Kislam.






Post a Comment

0 Comments