Mkurugenzi wa Msama Promotions ndg Alex Msama Amewaonya waimbaji wote wa nyimbo za injili Ambao wamekuwa wakishiriki kwenye majukwaa na wasanii muziki wa kidunia, kwani kufanya ivo ni kushiriki kwenye kumtukuza shetani.
Pia amewataka wasanii hao kuacha tamaa ya pesa ambayo inawapelekea wasanii hao kwenda kushiriki kwenye majukwaa ya muziki wa kidunia,
“Nawaonya waache kushiriki madhabahu za shetani,2 Wakorinto 6: 14-18 Msiambatane pamoja na watu wasioamini, pia wajihadhari na kupenda pesa kwani pesa nyingine ni za maagano ya kuzimu” Alex Msama
Alex Msama ni mdau mkubwa wa Muziki wa Injili na Hivi karibuni alipokea tuzo ya heshima ya kuwa muandaaji bora wa matamasha ya injili nchini Tanzania ambayo maarufu yalikuwa yanafahamika kwa jina la TAMASHA LA PASAKA
0 Comments