RAIS WA KENYA NA MWENYEKITI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI AWASILI TANZANIA

 




Na mwandishi wetu

Rais wa Jamhuri ya Kenya na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Mhe. William Samoei Ruto amewasili Nchini Tanzania  na kupokelewa na Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso.

Mhe. Rais Ruto amewasili kuhudhuria Mkutano wa Pamoja wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya za EAC na SADC utakaofanyika nchini tarehe 8 Februari, 2025.

Jumuiya zote mbili zinakutana kujadili namna ya kupata ufumbuzi kuhusu hali ya usalama Mashariki mwaJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.



Post a Comment

0 Comments