TAKUKURU TEMEKE YABAINI MAPUNGUFU KWENYE MRADI HUU WA BILIONI 1.6.

 



TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU)Mkoa wa Temeke imebaini mapungu kwenye mradi wa Bilioni 1.6 katika ujenzi wa ghorofa tatu unaojengwa katika Shule ya Sekondari Maganya wilayani Temeke mradi huo unatekelezwa na Mkandarasi Mbaza Engineering Campany Limited.

Hayo yamebainishwa mapema leo Jijini Dar es Salaam Naibu Mkuu wa TAKUKURU (M) Temeke,Isman Bukuku,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuzungumzia taarifa za Takukuru mkoani hapo.

Bukuku amesema katika robo ya pili ya mwaka 2024/2025 ilifanya ufuatiliaji kwenye miradi huo walishirikiana na wataalamu wa Manispaa ya Temeke kwa kuangalia jengo limejengwa kwa kiwango kilichokusudiwa na thamani ya fedha (value of Money) ya Serikali inaonekana.

"Katika ukaguzi huo maafisa wetu walibaini kuwa kuwa badala ya kutumia square piper zenye upana wa 2.5cm kutengeneza madirisha ya jengo hilo kama ilivyoelekezwa katika maelezo ya Gharama kazi,Mkandarasi alikuwa ametengeneza madirisha ya lengo hilo kutumia square pipes zenye upana wa 2.3 hali ambayo ni kinyume na maelekezo ya mradi 'huo "amesema Bukuku.

Aidha,Bukuku amesema Takukuru baada ya kubaini ya mapungu hayo ya vipimo vya Square Pipes walitoa maelekezo kwa msimamizi wa mradi ambaye ni Ofisi ya Mkurugenzi wa Temeke kupitia Mhandisi wa Manispaa hiyo kuwa Square Pipes zenye upana wa 2.3cm zilizotumika kujenga madirisha ya jengo husika zibadilishwe na badala yake ziwekwe zenye upana wa 2.5 cm kama ilivyoelezwa katika mradi huo.

Katika hatua nyingine Takukuru Temeke kwa kipindi cha robo wa mwaka wameendesha kazi ya kuimarisha klabu za wapinga rushwa kwenye vyuo vikuu na kati,shule za Sekondari na msingi,imefanya mikutano ya hadhara,uandishi wa makala mbalimbali zinahusu rushwa.

"Lengo kubwa ni kuzidi kuelimisha jamii kuhusu Rushwa na kuifanya jamii iweze kujua wajibu wake na namna inavyoweza kushirikiana na serikali katika kuzuia vitendo vya rushwa hasa kwenye miradi ya maendeleo."Amesema Bukuku,

Post a Comment

0 Comments