Na mwandishi wetu
Mwanazuoni maarufu barani Afrika, Profesa Patrick Lumumba, amewasili leo Mkoani Arusha kwa ajili ya kushiriki katika tukio kubwa la Jukwaa la Uchumi linalotarajiwa kufanyika kesho, tarehe 03 Mei 2025.
Jukwaa hilo linalenga kuchochea fikra mpya, ubunifu na ushirikiano wa wadau mbalimbali kwa lengo la kukuza uchumi wa wananchi wa Arusha na maeneo jirani.
Katika hotuba yake fupi mara baada ya kuwasili, Profesa Lumumba amesisitiza umuhimu wa kujenga uchumi unaotegemea maarifa, maadili na uzalendo.
0 Comments