Kaimu katibu mkuu kitengo cha afya Mr.Michael John ameongea na wandishi wa habari kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa kipindupindu kwa Tanzania Bara Taarifa iliyoandaliwa na waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,watoto na wazee Mh.Ummy Mwalimu "kasi ya ugonjwa wa kipindupindu imepungua kwa kipindi hiki cha mwenzi wa nne kwa 32% tofauti na mwenzi wa nane mwaka jana mpaka 17 mwenzi wa nne kulikuwa na wagonjwa 21,021 waliopatwa na ugonjwa kiasi cha kusababisha vifo vya watu 329.Mwenzi nne tarehe 18 mpaka 24 wagonjwa wamepungua kutoka kutoka 145 kwa mwenzi kufikia 142 kwa mwenzi kwa mikoa inayoongoza kwa sasa ni Morogoro ambapo wagonjwa 35 wameripotiwa kuugua ugonjwa huo kwa mwenzi huu,ikifatiwa na iringa hasa wilaya ya kilolo tofauti na awali ilikuwa ni iringa vijijini,mara wagonjwa 20,Dar es salaam wagonjwa 18,Manyara 21 hivyo takwimu zinaonyesha kushuka kasi ya ugonjwa huu kwa kipindi hiki hivyo wizara inaongeza juhudi za ziada ili kutokomeza kabisa ugonjwa huo"alisema kaimu
Pia aliongeza na kushauri Halmashauri,viongonzi,umma na wadau kuzingatia yafatayo nayo ni Waganga kutoa taarifa na taarifa sahihi za ugonjwa wa kipindupindu kwa kufuata muongozo wa wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia,watoto na wazee,Jamii kujenga vyoo salama,Upatikanaji wa maji safi na salama,Watu mashuhuri,viongozi na serikali za mitaa kuwajibika kuhamasisha umma juu ugonjwa huu wa kipindupindu na pia kuzingatia usafi wa chakula na matunda kabla ya kula.
Waziri wa wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia,watoto na wazee amefanya maamuzi ya kuongea na waandishi wa habari kila jamatatu wa wiki kwa ajili ya kutoa taarifa za mwelekeo wa ugonjwa wa kipindupindu,Hivyo leo ametoa taarifa hiyo iliyotolewa na kaimu katibu mkuu wa afya Mr. Michael john wizarani leo.
0 Comments