ADC YATAKA UWAZI MKATABA WA UWEKEZAJI BANDARI ZANZIBAR, CHAJIPANGA KUSHIKA DOLA 2025

 



Na  MWANDISHI WETU

CHAMA Cha Alliance Democratic Change (ADC) kimemuomba Rais wa Zanzibar ja Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hessen Mwinyi kuweka wazi mkataba wa uwekezaji wa Bandari ya Zanziber.

Ombi hilo limetolewa na Mwenyeki wa ADC Taifa Hamad Rashid akifungua Mkutano wa Bodi ya Uongozi ya Chama Taifa ambapo ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka uwazi wa mkataba wa DP World katika uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam.

“ADC tumeona, tunaomba uwazi uliofanyika kwenye mkataba na DP World, tunaomba uwazi huo huo ufanyike kwenye Mkataba wa uwekezaji wa Bandari ya Zanzibar,” amesema Rashid.

Katika hatua nyingine Rashid amewakaribisha Watanzania kujiunga na Chama hicho kwani kina sera zinazotekelezeka, kwamba matamanio yao ni kuona wananchi na Tanzania kwa ujumla wanaondokana na umasikini.

Kadhalika Rashid amempongeza Rais Samia kwa filamu yake ya Royal Tour kwani imezidi kuimarisha Sekta ya Utalii kwa kuongeza idadi ya watalii nchini.

Hata hivyo amesema kwamba pamoja na kuimarika kwa Utalii lakini bado haimnufaishi Mwananchi wa kawaida moja kwa moja, hivyo Serikali iangalie namba ya kufanya kila Mwananchi anufaike na ukuaji huo.

Kuhusu 4R za Rais Samia ameomba itolewe elimu ili ziweze kutekelezwa hadi ngazi za chini.

Mwenyekiti huyo amemuomba pia Rais Samia kuhakikisha mapendekezo ya kikosi Kazi kutekelezwa hususani tume guru ya uchaguzi ili uchaguzi ujao uwe wa huru na wazi na kuwezesha viongozi wanaostahili kushinda washinde.

Kutokana na vita vinavyoendelea baina ya Israel na Palestina ameomba Jumuiya za Kimataifa hususan Umoja wa Mataifa (UN) kuingilia Kati na kukomesha mgogoro huo.

Ameomba pande mbili hasimu kukaa meza moja na kupata Suluhu ya mgogoro huo.

Hivyo kutokana na vita hiyo ametoa tahadhari kwa viongozi kuhakikisha kila Wilaya inakuwa na Hifadhi ya chakula cha kutosha.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama hicho Doyo Hassan Doyo amesema Chama kimejipanga kuhakikisha kinashika Dola katika uchaguzi mkuu ujao wa 2025.

Kwamba wamedhamiria kukijenga Chama imara ambacho kitahakikisha kinaleta ushindani kwa vyama vingine.

Aidha Doyo amelaani kauli ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Paul Makonda kusema kwamba hakuna Vyama vya upinzani nchini.

“Tunalaani kauli ya Makonda kwamba hakuna Vyama vya siasa vya upinzani. Hii nidharau kwa Masajili wa Vyama vya Siasa,” amesema Doyo.

Doyo ameeleza kwamba kauli hiyo unakwenda kuvuruga nia njema ya 4R ya Rais Dkt. Samia.

Post a Comment

0 Comments