Na mwandishi wetu
KILE kinachoonekana sekta ya Benk nchini inazidi kukua,Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo, Dk Ibrahim Mwangalaba, amesema benki hiyo imepata ongezeko la faida kwa kipindi cha mwaka 2023 na kufikisha mtaji wa Sh bilioni 19.
Dk Mwangalaba amesema leo mapema jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi habari ambapo amesema hatua hiyo itawezesha benki kuongeza faida kwa fedha za wahisani kwa mwaka 2024 na kuboresha njia mbadala za upatikanaji wa huduma.
Hata hivyo,Dk Mwangalaba, amesema wako katika mazungumzo na Benki kuu ya Tanzania ili kupata kibali cha kufungua matawi mikoani kwa mwaka 2024 na kuifanya benki hiyo kuwa ya kitaifa.
“Benki imefikisha mtaji wa Sh bilioni 19 na kuiwezesha benki kufanya kazi nchi nzima na tunapanga kupanua huduma zetu kwa kufungua tawi moja na mawakala wapya 500 ambapo sasa kuna mawaka 1600 zaidi ya mikoa 11.
Amesema wamekuwa benki ya faida kwa miaka tisa tangu 2015 ilipoanzisha ambapo mwaka 2023 benki ilikuza faida kwa asilimia 66 baada ya kodi na faida baada ya kodi iliongezeka hadi Sh bilioni 2.3 kutoka Sh bilioni 1.4 ya mwaka 2022.
“Ubora wa mikopo umeimarika kutoka mikopo chechefu asilimia 5.2 mwaka 2022 hadi asilimia 4.95 mwaka 2023,amana za wateja zimeongezeka kwa asilimia 15 kutoka Sh bilioni 78 mwaka 2022 hadi Sh bilioni 90 mwaka 2023.
Amesema pia mikopo kwa wateja imeongezeka kwa asilimia 21 kutoka sh bilioni 61 mwaka 2022 hadi Sh bilion,74 mwaka 2023.
Aidha ameeleza kuwa mtaji wa benki umeimarika kwa asilimia 12 kutoka Sh bilioni 17 mwaka 2022 hadi Sh bilioni 19 mwaka 2023.
“Tumefungua tawi jipya Mbagala ambalo ni tawi letu la tano tukiwa na lengo la kuwasogezea huduma kwa wateja,”amesema
0 Comments