Na mwandishi wetu
KATIBU Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi *(CCM)*, Ally Salum Hapi *(MNEC)* amewataka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo *(CHADEMA)* kuacha kulalamika na badala yake kuelekeza nguvu zao katika kuwasilisha na kueleza ajenda za maendeleo kwa wananchi.
Hapi alitoa kauli hiyo katika mkutano wa wa uzinduzi wa kampeni za Serikali za Vijiji, Vitongoji na Mitaa za Chama Cha Mapinduzi *(CCM)* uliofanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Mjini katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kashai Mkoani Kagera huku akisisitiza umuhimu wa siasa za hoja zenye tija kwa maendeleo ya taifa, na kusema kuwa malalamiko ya mara kwa mara hayaleti manufaa yoyote kwa wananchi kwani wananchi hawahitaji kusikia porojo wanataka maendeleo.
Hapi aliongeza kuwa badala ya kuendelea kulalamika, vyama vya upinzani vinapaswa kuonyesha mfano kwa kueleza mipango na mikakati yao ya kuleta maendeleo kwa jamii.
*#WazaziTukoMstariWaMbeleUchaguziWaSerikaliZaMitaa2024*
*#WazaziMpangoMzimaNaRaisDkt.SamiaSuluhuHassan2025*
*#MwanaUmleavyo,NdivyoAkuavyo*
*#UchunguwaMwanaAujuayeMzazi*
*#WazaziTukoImara*
*#WazaziNaSamia2025*
*Imeandaliwa na Idara ya Oganaizesheni ya Jumuiya ya Wazazi Taifa*
0 Comments