20 NOV 2024
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Komred Nape Nnauye ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama amesema Chama Cha Mapinduzi kina sababu za kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 kwa sababu Mwaka 2019 mlikiamini na kukipa ridhaa Chama Cha Mapinduzi kushinda uchaguzi wa serikali za Mitaa kwa asilimia kubwa, na kuongoza serikali hadi leo tunaporudi tena kuomba kura kwa mara nyingine tena.
“Hii ni sababu inayotofautisha Chama Cha Mapinduzi na Vyama vingine, hivyo endeleeni kukiamini Chama Cha Mapinduzi kama mlivyokiamini mwaka 2019 na sasa tumerudi kuwaeleza yale tuliyoyafanya na kwanini tunaomba tena ridhaa ya kuongoza katika ngazi ya Mitaa, Vijiji na Vitongoji 2024” _Amesema Komred Nape_
Aidha komred Nape amewasisitiza viongozi waliochaguliwa kwenda kupeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi, wafanye kampeni za kisayansi na kistaarabu bila kuwatukana vyama vingine.
“Wakiwashambulia kwa matusi waacheni kwa sababu wameshaanza wenyewe kupasuana ndani kwa ndani na muda siyo mrefu watagawana Mbawa” _Amesema Komred Nape_
“Ndugu wananchi na wanachama pamoja na viongozi tunaomba mkakichague Chama Cha Mapinduzi kwa sababu hakuna Chama kingine kinachoweza kuwaongoza na kuwaletea maendeleo wananchi isipokuwa Chama Cha Mapinduzi pekee, huko kwingine wanagombana ivi karubuni watagawana Mbawa” _Amesema Komred Nape._
Komred Nape ameielekeza Serikali kuweka utaratibu mzuri wa kuwalipa wananchi fedha zao zaidi ya Bilioni 21 ndani ya mwezi huu wanazodai kwenye Mfuko wa shirika la NFRA linalojishughulisha na ununuzi wa mazao hapa Rukwa.
“Nimeongea na waziri wa Kilimo Ndg. Bashe amenihakikishia ndani ya mwezi Novemba atawalipa wakulima na wafanya biashara wa Mahindi ambao wanadai madai yao tangu walipouza mazao yao na kutokulipwa hadi sasa, na zoezi la ununuzi litaendelea hadi Mwezi Februari 2025” _Amesema Komred Nape._
Pamoja na mambo mengine Komred Nape akiwa katika Mkoa wa Rukwa wilaya ya Sumbawanga Mjini amezindua Shina la kikundi cha Umoja wa Madalali wa Maroli Sumbawanga.
#Kaziiendelee
#rukwayasamia
#mitanotenaSamia
0 Comments