Na mwandishi wetu
Tamasha la Samia Fashion Festival awamu ya pili linatarajiwa kufanyika Zanzibar Novemba 30/2024 likiwa na lengo la kukuza ubunifu pamoja na heshima ya mtanzania.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam Mwanzilishi wa Tamasha hilo Hadija Mwanamboka amesema tamasha hilo ni katika kuendeleza ubunifu wa mavazi ya stara na kukuza maadili ya kitanzania.
Amesema kuwa kupitia tamasha hilo pia wataweza kuwasaidia watoto wanaoishi na virusi vya ukimwi.
Kwa upande wake Mwanamitindo wa Kimataifa Millen Happiness Magese ambaye ni jaji Mkuu katika tamasha hilo amesema uandaaji wa vazi la Samia ni ubunifu na stara ambayo inafaa kuwekwa kwenye makumbusho ya taifa na kuwa sehemu ya kihistoria na kukumbukwa na kizazi kijacho
Amesema amekuwa mwanamitindo wa Kimataifa Kwa muda mrefu hivyo anaamini kuwa ushindi hio utakuwa umekidhi sifa zote zinazotakiwa akishirikiana na jopo lote la majaji akiweno Mwigizaji Idrisi Sultan, Joket, Martini Kadinda, Faraja Nyarandu, Nancy Sumari.
Hata hivyo amewataka Watanzania kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais Dkt.Samia anazofanya kuhakikisha kuwa kazi ya Sanaa na ubunifu inafanya vizuri na wao kama Wana tasnia ya mtindo watashirikiana kuhakikisha inafanya vizuri.
Naye Mwigizaji Idrisi Sultan amewasisitiza watanzania kuendelea kuwaaunga mkono Wanawake katika kufikia ndoto.
0 Comments