Update kutoka Tandahimba: Kampeni za Uchaguzi za Chama cha NLD Zinaendelea Kwa Kasi
Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Wilayani Tandahimba kupitia Mgombea wa Chama cha NLD, Ndugu Karimu Hamisi Dadi (maarufu kama Washoka), zinaendelea kwa nguvu. Wananchi wa Kata ya Nanhyanga, hasa Kijiji cha Nanhyanga A na Mtaa wa Miembeni, wameonyesha kuhamasika na kumuunga mkono mgombea huyo katika azma yake ya kuleta mabadiliko ya kweli katika kijiji chao.
Ndugu Hamisi Dadi anajitahidi kuwasiliana na wananchi moja kwa moja kupitia kampeni za nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa, na kijiwe kwa kijiwe. Katika mikutano yake, amekuwa akihimiza wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi, huku akiwahimiza wananchi kwa kusema: "Wananchi msifanye makosa miaka 4 ni mingi sana, msijaribu kuweka rayani maisha yenu, chagueni viongozi sahihi kwenu, mimi nimejizatiti kuwatumikia."
Kwa sasa, kampeni za mgombea huyo zinaendelea vizuri Kijiji kwa kijiji na wananchi wameonyesha kuhamasika na kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hiyo kesho, tarehe 27 Novemba 2024.
*By Ombe B. Kilonzo*
0 Comments