𝗦𝗢𝗞𝗢 𝗟𝗔 𝗞𝗜𝗦𝗔𝗦𝗔 𝗖𝗛𝗨𝗪𝗜𝗡𝗜 𝗞𝗨𝗟𝗘𝗧𝗔 𝗠𝗔𝗣𝗜𝗡𝗗𝗨𝗭𝗜 𝗠𝗔𝗞𝗨𝗕𝗪𝗔 𝗞𝗪𝗘𝗡𝗬𝗘 𝗨𝗞𝗨𝗔𝗝𝗜 𝗪𝗔 𝗨𝗖𝗛𝗨𝗠𝗜 𝗪𝗔 𝗭𝗔𝗡𝗭𝗜𝗕𝗔𝗥 - 𝗖𝗣𝗔 𝗠𝗔𝗞𝗔𝗟𝗟𝗔

 



Na mwandishi wetu

Katibu wa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu CPA Amos Makalla amesema Soko la kisasa la Chuwini litaleta Mapinduzi makubwa ya kiuchumi kwa wananchi Zanzibar.

Amesema hayo leo Ijumaa 31.01.2025 alipokuwa akikagua mradio huo wa kimkakati kwenye muendelezo wa ziara yake ya mikoa sita ya kichama visiwani Zanzibar.

Amesema kuwa soko hilo kubwa zaidi ya soko la kariakoo jijini Dar es Salaam kwani litachukua zaidi ya Wafanyabiashara Elfu Nne kwa wakati mmoja ambapo lile la Kariakoo litachukua wafanyabiashara kati ya 3000-3500.

Aidha amepongeza ubunifu wa kuchanganya soko pamoja na kituo cha mabasi kwa itasaidia sana kukua kwa biashara.

"Nami nijumuike nanyi kuwa kuwapongeza Viongozi wetu dkt Samia na Dkt Hussein Mwinyi kwa namna wanavyoshirikiana katika kuwaletea maendeleo nilikuwa naona tu kwenye Mitandao nimejionea soko kubwa la kisasa kabisa na kubwa na kupitia hili nimeshawishika kwanini Wajumbe waliamua dkt Samia na Dkt Mwinyi wawe wagombea wa Urais Mapema"

"Kwani hapa mmeweka historia kutoka Bonde la mpunga mpaka soko la kisasa sasa wale Zambarau wenye miwani za Mbao waje wajionee kazi ilivyofanyika kwani kuona ni kuamini” alisema




Post a Comment

0 Comments