RAIS WA KWANZA WA NAMIBIA SAM NUJOMA AFARIKI DUNIA

 




Na mwandishi wetu

Sam Nujoma, Baba wa Taifa la Namibia na Rais wa kwanza wa nchi hiyo, amefariki dunia Februari 8, 2025, akiwa na umri wa miaka 95. Taarifa ya kifo chake imetolewa na Rais wa sasa wa Namibia, Nangolo Mbumba 

Nujoma aliongoza harakati za ukombozi kupitia Chama cha SWAPO, akipigania uhuru wa Namibia na kuwa Rais wa kwanza wa taifa hilo huru mnamo Machi 21, 1990, akihudumu kwa mihula mitatu hadi 2005. 

Katika uongozi wake, Nujoma alijenga misingi ya taifa jipya kwa kuanzisha katiba ya kidemokrasia na kuhimiza maridhiano ya kitaifa. Alijulikana kwa msimamo wake mkali dhidi ya ukoloni na ubaguzi wa rangi, lakini pia alihimiza umoja na mshikamano miongoni mwa Wanamibia wote. 

Kwa mchango wake mkubwa katika harakati za ukombozi na ujenzi wa taifa, Nujoma atakumbukwa kama kiongozi shupavu na mzalendo wa kweli. Mchango wake utaendelea kuishi katika historia ya Namibia na Afrika kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments