-Amshukuru Rais Dkt Samia kwa namna anavyoendelea kuimarisha TRA
-Asema Kodi inayolipwa inaonekana hususani DSM miradi mingi ya maendeleo inatekelezwa kwa mfano mradi wa ujenzi wa barabara za mwendokasi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila wakati wa hafla ya ugawaji tuzo kwa walipa kodi wa Mkoa huo iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika ukumbi wa Mlimani City.
RC Chalamila ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo amesema kodi ni jambo la msingi na lazima hivyo ni vema jamii ikatambua umuhimu wa kila mmoja kulipa kodi kulingana na kipato chake ambapo ameitaka TRA kuendelea kutoa elimu ya kodi kwa umma ili kodi ikusanywe bila manung'uniko watu walipe kwa hiari.
Aidha RC Chalamila amemshukuru Rais Dk Samia kwa kuendelea kuimarisha Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kuwa sasa kodi imekuwa ikikusanywa bila manung'uniko lakini pia pesa nyingi zimeendelea kutolewa na Mhe Rais Dkt Samia miradi mingi inatekelezwa katika Mkoa wa Dar es Salaam "Kodi inayolipwa inaonekana" Alisema RC Chalamila
Vilevile amewataka watanzania kudai risiti wanapofanya manunuzi, kujiepusha na vitendo vya ukwepaji kodi, wafanya biashara walipe kodi kwa hiari bila shuruti.
Kwa upande wa Kamishna Mkuu wa TRA Bwana Yusufu Mwenda amesema DSM inachangia kwa kiasi kikubwa pato la Taifa hivyo amesema TRA itaendelea na mapambano ya biashara za magendo, kuendeleza utulivu wa kibiashara katika Mkoa pia kuwekeza kwa watumishi TRA vilevile kuweka mazingira rafiki kwa mlipa kodi
Mwisho RC Chalamila aligawa tuzo kwa washindi mbalimbali ambao wamekidhi vigezo vya kuwa walipa Kodi bora.
0 Comments