TAMASHA LA KUOMBEA UCHAGUZI MKUU 2025 KUANZA KURINDIMA DAR KISHA MIKOA 26

 


Na mwandishi wetu

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Kuombea  uchaguzi mkuu  2025 ndugu Alex Msama leo ameongea na wandishi wa habari kuwa Maandalizi ya Tamasha la kuombea uchaguzi yanaendelea vizuri na  kuwa Tamasha hilo lipo na litafanyika katika jiji la Dar es Salaam na baadae kufanyika Mikoa 26 ya Tanzania

Ameyasema hayo leo alipongea na waandishi wa Habari kuhusiana na maandalizi ya Tamasha hilo. “Maandalizi ya tamasha yanaendelea vizuri na tunakaribisha wadhamini kuja kusaidia kufanikisha Tamasha hili kubwa ambalo litafanyika Mikoa yote ya nchi yetu ya Tanzania tukianzia  na Mkoa wa Dar es Salaam.  Ndugu Alex Msama Mwenyekiti wa Kamati ya Mandalizi ya tamasha hilo amesema kwasasa jambo kubwa linalofanyika ni kuendelea kuzungumza na wafadhili na tukifanikiwa tu kupata wadhamini basi tamasha  litakuwa halina kingilio litakuwa bule. 

Tamasha la Kuombea  uchaguzi litafanyika hivi karibuni na kuwaunganisha waimbaji mbali mbali wa nyimbo za injili Ndani na Nje ya Tanzania.

Post a Comment

0 Comments