Na mwandishi wetu
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Machi 11, 2025 Jijini Dar Es Salaam amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Burundi nchini Mhe. Leontine Nzeyimana
Katika Mazungumzo yao viongozi hao wamejadiliana mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya Sheria ikiwemo ushirikiano katika kupambana na uhalifu, na masuala ya haki za binadamu baina ya mataifa hayo mawili.
Ikumbukwe kuwa Tanzania na Burundi zimekuwa na uhusiano wa karibu na ushirikiano wa muda mrefu, tangu enzi za waasisi wa mataifa hayo ambapo urafiki wa kidiplomasia umejengwa juu ya msingi wa historia, tamaduni zinazoendana, na maslahi ya pamoja.
0 Comments