DC GEITA AWAONDOA HOFU WALIOFIKWA NA MAPOROMOKO YA UDONGO.


 Na mwandishi wetu

Ikiwa ni siku moja tu tangu kuripoti habari ambayo inahusu maporomoko ya udongo ambayo yametokea Kwenye Mtaa wa Nshinde Kata ya Nyankumbu Wilayani Geita,Kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na mkuu wa Wilaya hiyo,Hashimu Komba imefika kwenye eneo ambalo limeathirika kwaajili ya kujionea uharibifu ambao umetokea.


Akiwa kwenye eneo hilo ambalo mashamba takribani ekari 6 ambazo zimeharibiwa kwa kufunikwa na udongo mazao yake ,Mkuu wa Wilaya ya geita Hashimu Komba amewasikiliza wananchi ambao wameelezea namna ambavyo hali hiyo ilivyotokea.


“Kuna kitu kinaitwa kimbunga kinatoka juu ndicho kilichopiga hapa chini na kusababisha hali hii ambayo Mkuu wa wilaya umeiona maana hapa kuna kijana ambaye alikuwa analinda mpunga wangu ambao ulikuwa umebakiza wiki 2 nianze kuvuna lakini kitu cha kushangaza nilikuta wote umefunikwa na udongo ,kweli unapoona hapa wala sio sijui ni mpasuko wa kawaida hapana hapa ni kile kimbunga ambacho kinatoka juu kwa kasi kubwa”Mahandamano Ezekiel Mkazi wa Nshinde.


“Hii hali imejirudia mara ya pili sasa mwaka 1998  palilipuka tena nayakafanya maporomoko makubwa zaidi ya haya nawaza eneo hili kuna nini kwanini iwe inajirudia au sehemu hii kuna miamba gani inayosababisha maporomoko kila mara maana pia kipindi hicho yaliyoka maji mengi sana”Hussein Masaganya Mkazi wa Nshinde.


Kwa upande wake Mjiolojia kutoka mgodi wa dhahabu wa Geita GGML,Mussa Kasano,ameelezea chanzo ambacho kimepelekea maporomoko hayo ni maji kuzidi kwenye ardhi na kushindwa kuimili hali hiyo.


Mkuu wa wilaya ya Geita,Hashim Komba amewaondoa hofu wananchi kuwa ardhi hiyo inawingi wa maji ndio chanzo kilichosababisha maporomoko na kwamba hakuna mlipuko wowote ambao umejitokeza.


“Kwenye eneo hili ambacho kimejitokeza ardhi hii imejaa maji ya kutosha na ushuhuda tumeupata kwa mzee wetu amesema mwaka 1998 hali hii ilijitokeza jambo la kwanza tutakwenda kuwashirikisha wataalamu wa miamba wa ndani ya serikali hili waje wafanye tafiti za kutosha kuhusiana na eneo hili lakini kwa hoja ya kwamba ni mlipuko wote tumepata majawabu kwamba hakuna mlipuko uliojitokeza”Hashim Komba Mkuu wa wilaya ya Geita.









Post a Comment

0 Comments