MAKALLA: MSIWACHAGUE WAPINZANI HAWAAMINIANI NA HAWAAMINIKI.

 


*MAKALLA: MSIWACHAGUE WAPINZANI HAWAAMINIANI NA HAWAAMINIKI.*


KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla amesema vyama vya upinzani haviaminiki, wala viongozi wao hawaaminiani, hivyo wagombea wake hawastahili kuchaguliwa. 

Makala amesema hayo wakati akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, katika Kata ya Manzese, Jimbo la Ubungo, jijini Dar es Salaam, leo tarehe 24 Novemba 2024.

CPA Makalla alitoa wito kwa wananchi kuwachagua wagombea wa CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

Makalla alisema vyama hivyo vya upinzani haviwezi kuaminiwa kupewa nafasi ya kuongoza mitaa, vijiji wala vitongoji, kwa sababu viongozi wake hawana uadilifu. 

"Hela tu ya majimbo walikuwa wanatafuna hawa ndiyo uwape mitaa hiyo mihuri itakuwa salama? 

"Hawaaminiki wa lolote na wao wenyewe hawajiamini. Mwaka 2020 walipata wabunge 19 wa viti maalum, lakini wakawatimua, mna uhakika gani hawa wenyeviti wakichaguliwa kama hawatawatimua?," alihoji CPA Makalla.

Alisisitiza: "Wabunge wao wakawapa jina baya COVID 19 lakini licha ya kuwapa jina baya lakini ruzuku wanachukua."






Post a Comment

0 Comments