TANZANIA YASHINDA TUZO YA KUONGOZA DUNIANI KWA SAFARI ZA WATALII

 



Na mwandishi wetu

Tuzo iliyotolewa kwa nchi ya Tanzania kwa kuyashinda mataifa mbalimbali baada ya kuibuka mshindi katika eneo linaloongoza zaidi duniani kwa utalii wa safari (hasa za kuona Wanyama wa porini) hatimaye imewasili nchini kupitia Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Novemba 26, Novemba 2024.

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi akipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Ephraim Mafuru amewasili na tuzo hiyo iliyotolewa Novemba 24, 2024 Kisiwani Madeira, Ureno ikiwa tuzo hiyo ni ushahidi wa matokeo ya uhifadhi mkubwa wa nchi uliofanywa na Serikali chini ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na uwekezaji mkubwa katika kutangaza utalii.

Tuzo hiyo ndio tuzo ya juu zaidi duniani na tangu mwaka 1993 utoaji tuzo umekuwa ukitambua mafanikio na umahiri katika ngazi ya mabara na kidunia katika kategoria anuai za Utalii.






Post a Comment

0 Comments