DK.MWINYI AWASILI DODOMA

 





Na mwandishi wetu

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar , Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amewasili Dodoma  kuhudhuria Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 48 ya Kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi .

Alipowasili Uwanja wa Ndege wa Dodoma Dk.Mwinyi alipokelewa na  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi  wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt, Mohamed Said Dimwa .

Kilele cha Sherehe hizo zitafanyika kesho tarehe 05 Februari 2025 katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Post a Comment

0 Comments