KAMATI YA BUNGE YAKAGUA MRADI WA NYUMBA NSSF MTONI KIJICHI, KIKWETE ASIFU USTAHIMILIVU NSSF.

 


Na mwandishi wetu

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii wametembelea na kukagua Mradi wa Nyumba za Mtoni Kijichi awamu ya Tatu unaomilikiwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) leo Machi 16, 2025 Jijini Dar es salaam.

Akizungumza Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Fatma Toufiq amesema Kamati hiyo imeridhishwa na kupongeza uwekezaji huo wenye tija ambao utawezesha wakazi wa jijini Dar es Salaam kupata makazi bora yaliyopo katika mradi huo.

Aidha, amehimiza uwepo Zahanati, Maduka na maeneo ya michezo kwa ajili ya watoto katika eneo hilo ili wapangaji waweze kupata huduma mbalimbali za kijamii kwa karibu.

Awali akizungumza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete, amesema NSSF imeendelea kuwa stahimilivu kwa kusajili idadi kubwa ya Wafanyakazi kwenye sekta binafsi. 

Naye Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba amesema mradi wa Nyumba wa Mtoni Kijichi tayari umetoa makazi kwa familia 390 ambapo nyumba zimenunuliwa.

Pia, amesema idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka na kufikia familia 1,105 pindi nyumba zote zitakapo kamilika na kuuzwa, hivyo kuchangia katika kupunguza uhaba wa makazi kwa wakazi wa Dar es salaam.










@owm_tz 

@onwm_tanzania 

@bunge.tanzania

@ridhiwani_kikwete 

@patrobasskatambi_ 

@venusnyotah 

@nssftz 

@msemajimkuuwaserikali

Post a Comment

0 Comments