MWAMBENE AKAGUA VIWANJA VYA MICHEZO IRINGA

 




Na mwandishi wetu


Ikiwa ni maadalizi ya Mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Bw. Atupele Mwambene, Machi,15,2025 amewasili mkoani Iringa kwa lengo la kufanya ziara ya kukagua viwanja vitakavyotumika kwaajili ya michezo na sehemu za  malazi.

Akiwa katika ziara hiyo Bw. Mwambene amepongeza maandalizi ya mashindano hayo yanayofanywa na wadau mbalimbali kwa kushirikiana bega kwa bega na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa iringa  ambapo Bw. Mwambene ametembelea katika shule ya Wasichana Ya Iringa, Shule ya Sekondari Kreluu,Chuo cha Uwalimu cha Kreluu,Uwanja Wa Kichangani pamoja na Shule ya Sekondari ya Lugalo.

Mashindano hayo kitaifa yanatarajia kufanyika mkoani hapa kuanzia Juni,08-Julai 04,2025.





Post a Comment

0 Comments