🗓️16-03-2025
📍GEITA
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya UVCCM Taifa Ndugu Rehema Sombi Omary (MNEC) ameongoza Matembezi ya Amani ya Kumuenzi Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Kwa Kutimiza Miaka Minne Tangu Kufariki.
Hafla hiyo imefanyika leo Machi 16, 2025 Wilayani Chato Mkoani Geita ambapo Makamu Mwenyekiti mwenyekiti Amewaongoza Vijana wa Mkoa wa Geita katika Matembezi hayo yaliyoambatana na Kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato.
Akiwa Hospitalini hapo wameshiriki katika zoezi la uchangiaji Damu, na Kuwatendea Matendo ya Huruma Wagonjwa na kutembelea Wodi ya watoto waliozaliwa hospitalini hapo na Kuwakabidhi Mahitaji mbalimbali yaliyoandaliwa na familia ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli wakiwakilishwa na Mwanafamilia Jessica Magufuli.
Aidha Ndugu Rehema ameshiriki katika Sala fupi na Dua ya kumuombea Hayati Dkt. John Pombe Magufuli iliyofanyika katika nyumba yake ya milele Katika kijiji cha Mlimani Wilayani Chato.
Akizungumza na Maelfu ya Vijana Waliojitokeza Katika Hafla hiyo, Komredi Sombi Amesema UVCCM itaendelea Kumuenzi na Kumkumbuka Hayati John Magufuli Kwa Mchango wake Mkubwa Alioutoa Katika Kulijenga Taifa La Tanzania wakati wa Uhai wake akiwa Madarakani.
Pia Amempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza mema na mazuri yote yalivyoasisiwa na mtangulizi wake.
Kumbukizi ya Kumuenzi Hayati Dkt John Pombe Magufuli Imeandaliwa na Familia Kwa kushirikiana na UVCCM Mkoa wa Geita, Imefanyika Wilayani Chato Mkoa wa Geita , Na kuhudhuriwa na Viongozi Mbalimbali Mbalimbali wa Chama na Serikali.
Mgeni Rasmi katika Hafla hiyo ni Ndugu Rehema Sombi Omary (MNEC) Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya UVCCM Taifa.
#Miaka4YaMagufuli
#PumzikaKwaAmaniJPM
0 Comments