Na mwandishi wetu
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndg. Mohammed Ali Kawaida (MCC) ameshiriki Iftar na Dua Maalum pamoja na Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa UVCCM Vyuo na Vyuo Vikuu katika Ofisi za Makao Makuu ya UVCCM Taifa Dodoma.
Iftar hiyo pia imehudhuliwa na watumishi wa UVCCM Makao Makuu Dodoma ambapo Ndg. Kawaida amewashukuru wote kwa kushiriki na kuwataka kuendelea kuzingatia yote yanayoelekezwa katika mwezi mtukufu wa Ramadhan.
#KazinaUtuTunasongaMbele
#TunazimaZoteTunawashaKijani
0 Comments