Na mwandishi wetu
Katibu Mkuu wa UVCCM, Ndg. Jokate Urban Mwegelo amekabidhi zawadi ya vitenge kwa watumishi wote Wanawake wa UVCCM.
Ndg. Jokate ambaye ni Katibu Mkuu wa Kwanza Mwanamke wa UVCCM amekuwa mfano wa kuigwa kwa Mabinti wengi nchini kujiunga katika nafasi mbalimbali za uongozi na siasa amefanya zoezi hilo leo tarehe 06 Machi 2025 katika Makao Makuu ya UVCCM Dodoma kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani tarehe 08 Machi 2025 ambayo kitaifa yatafanyika jijini Arusha na Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kauli Mbiu ya maadhimisho ya mwaka 2025 ni; "Wanawake na Wasichana 2025 tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji"
#BintinaSamia
#TunazimaZoteTunawashaKijani
0 Comments