Na mwandishi wetu
WANANCHI wa Mtaa wa Faru, Kata ya Mnyamani, wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam, wameiomba serikali kuwapa msaada wa dharura baada ya maji ya mvua yenye oili chafu kufurika katika nyumba zao na kuharibu mali.
Wakizungumza katika eneo hilo, wananchi hao wamesema adha hiyo imechangiwa na mndarasi anayejenga Babara ya Faru , kuto kuweka mifareji hivyo kufanya maji mengi ya mvua iliyonyesha alfajiri ya leo kuongoia katika nyumba zao na kuwaletea adha kubwa.
Mkazi wa eneo hilo, Lilian Mwakatuma, alisema jana mkandarasi anayejenga Barabara ya Faru alimwaga oili chafu katika barabara hiyo lakini baada ya mvua kunyesha maji yaliyochanganyika na mafuta hayo vilingia ndani na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali zao.
“Chakula kimeharibika, vyombo vya ndani, vitanda, magodoro, vyombo vya jikoni vyote vimetapakaa mafuta. Tunaomba msaada wa dharula kwa sababu hata magodoro yamelowa,”amesema Liliani.
Diwani wa Kata hiyo Shukuru Dege, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba tayari wamewasiliana na Mkandarasi Kampuni ya Southern Link kuchukua hatua za kufyonza huku wakiwasiliana na kitengo cha maafa kwa hatua zaidi.
0 Comments