TCRA:SEKTA YA USAFIRISHAJI WA VIFURUSHI,VIPETO NA NYARAKA ZINA MCHANGO MKUBWA KUPITIA MFUMO WA KIDIGITALI

 


Afisa Mwandamizi kutoka TCRA,Abel John


Na mwandishi wetu kutoka Arusha

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imetoa elimu ya urasimishaji wa huduma za usafirishaji mizigo,vipeto na nyaraka kwa wadau wa usafirishaji Kanda ya Kaskazini ikiwa ni kuelekea katika kampeni ya uhamasishaji wa usajili na upataji wa leseni ya usafirishaji.

Akizungumza katika warisha iliyofanyika jijini Arusha,Afisa Mawasiliano na Mahusiano kwa Umma kutoka TCRA Bwn.Semu Mwakyanjala amesema kuwa sekta ya usafirishaji wa vifurushi,vipeto na nyaraka inamchango mkubwa hapa nchini kutokana na huduma hizo kupitia kwenye mfumo wa kidigiti.

Aidha amesema kuwa sekta hiyo imepita katika maboresho na kuongeza idadi ya watoa hudum wa vifurushi,vipeto na nyaraka na kufikia zaidi ya 96 ukijumlisha na shirika la Posta lenyewe hali inayopelekea wananchi walio wengi kunufaika.

Ameongeza kuwa kutokana na baadhi ya watoa huduma kutoa huduma za vifurushi na vipeto bila leseni,serikali kupitia TCRA inaendelea kuhamadisha watoa huduma hizo ambao hawajasajiliwa kurasimisha huduma zao ili waweze kuhudumia wananchi kwa ufasaha.

Vilevile amewata watoa huduma wenye leseni kuzingati masharti ya leseni ya TCRA kwani zipo baadhi ya huduma au bidhaa ambazo haziruhusiwi kusafirishwa kwenye mabasi ya abiria hususani zile ambazo zinaasili ya kilipuka.

Kwa upande wake Afisa Mwandamizi kutoka TCRA,Abel John amesema kuwa serikali imekusudia kuweka utaribu katika maeneo ya usafirishaji kwa kuangalia haki ya mtumaji na msafirishaji wa vifurushi,vipeto na nyaraka ambapo amewataka wasafirishaji kuhakikisha kile kinachosafirishwa hakileti madhara kwa abiria.

John ameeleza lengo la warisha hiyo kuwa ni ili kuhamasisha wananchi kuhakikisha wanatumia huduma za usafirishaji wa vifurushi na vipeto kwa kutumia wasafirishaji waliosajiliwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania.

"Wananchi wakisafirisha vifurushi na vipeto kwa kutumia wasafirishaji waliosajiliwa inawasaidia kuhakikisha wanapata haki zao endapo kutatokea changamoto zozote katika usafitishaji."alisisitiza Afisa Mwandamizi kutoka TCRA,Abel John

Ameongeza kuwa hasa usafirishaji wa vifurushi na vipeto kwa kutumia mabasi ya abiria,posta na makampuni ya Kurya umeongezeka kutokana na fursa zilizotolewa na kuongezeka kwa digitali,wananchi wanaweza kuagiza mizigo yao kutumia njia ya tandao.

Sambamba na hayo amesema kuwa kutokana na kuangalia suala la usalama,watahakikisha kwamba havisafirishi vitu ambavyo haviruhusiwi kwa kutumia wasafirishaji ambao hawajasajiliwa.

Arusha,Afisa Mawasiliano na Mahusiano kwa Umma kutoka TCRA Bwn.Semu Mwakyanjala



Post a Comment

0 Comments