MAHAFALI YA SITA SHULE YA AWALI NA MSINGI (SAFI SCHOOLS) YAWEKA REKODI

 




 *SEPTEMBA* 21 .2024 shule ya awali na msingi(Safi schools) iliyopo jijini Dar es salaam wilaya ya Ubungo imefanya mahafali yake ya Sita tokea shule hiyo isajiliwe rasmi mnamo mwaka 2017 


Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi mkuu wa shule hiyo Ndg.Amani Soko amesema mahafali ya mwaka huu yamefanyika kwa kishindo na imekuja wakati ambao shule imefanikiwa katika maeneo kadhaa ya kielimu na michezo ikiwemo ongezeko la ufaulu wa somo ya Hisabati ,Sayansi ,Kuzingatia maadili na  kusajili academy itakayokua inakuza vipaji (Safi Sports academy) 


Mkurugenzi pia ametoa wito kwa walimu wa shule yake na kote nchini kuhakikisha wanafundisha Wanafunzi kwa vitendo zaidi ili waache kukariri kwani linapokuja suala la interview/mahojiano wakati wanatafuta ajira wanakua wanakosa vigezo kwakutoingia kwenye ushindani wa ajira 


Hatahivyo ametoa rai kwa wazazi na wanafunzi wa watoto wanaohitimu shule za msingi nchini kulinda maadili ya watoto wao ambao kimsingi wengi wao waliomaliza darasa la saba wapo katika kipindi cha mpito chenye ushawishi mwingi 


Kwa upande wake mwanafunzi aliyehitumu Darasa la saba katika shule hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Evania Faustine ameushukuru uongozi wa shule hiyo kwa kumpatia malezi bora ya elimu na amewakumbusha wahitimu wenzake kua wajilinde ,wajitunze na wawe na maadili mema watakaporudi majumbani


Aidha Shule hiyo bado inafanya vizuri katika wilaya ya Ubungo ambapo imekua ikiingia kwenye chati za kumi bora mara kadhaa pia kushika nafasi tofauti ikiwemo nafasi ya 4 ,5 na sita






























Post a Comment

0 Comments