COSTECH YAZINDUA MIONGOZO 4 YA UBUNIFU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA

 





Na mwandishi wetu

Tume ya Taifa ya sayansi na teknolojia (COSTECH)Leo imezindua miongozo minne itakayowawezesha uratibu katika masuala ya sayansi na teknolojia na ubunifu.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa miongozo hiyo iliyofanyika leo Oktoba 4,2024 jijini Dar es salaam katibu mkuu wa wizara ya elimu,sayansi na teknolojia Bi Carolyne Nombo amesema miongozo hiyo itakuwa chachu ya ukuaji wa sayansi teknolojia ya ubunifu.

Amesema miongoni mwa miongozo hiyo ni pamoja na muongozo was ubunifu (innovation framework)ambao utasaidia hasa katika tafiti za kibunifu hapa nchini na umelenga pia kuwalinda wabunifu na watafiti wa Tanzania kupitia tafiti wanazozifanya.

"Najua kumekuwa na Sheria ya data sharing kwa hiyo tunataka tuwalinde wabunifu na watafiti wetu katika taarifa wanazozalisha lakini pia kuwe na mfumo mzuri wa kuweza kusambaza taarifa na tafiti ambazo wanazizalisha na namna ambavyo tunahusiana watafiti mbalimbali ikiwemo watu wa vyuo vikuu na tasnia ya ubunifu kupitia teknlojia" amesema.

Aidha ameongeza kuwa uwekezaji uliofanywa na serikali ya awamu ya sita  kupitia sayansi na teknolojia kwani hakuna nchi yoyote itakayoendelea bila kuwa na matumizi makubwa ya sayansi,teknolojia na ubunifu na Tanzania imepiga hatua na kupitia miongozo iliyozinduliwa Sasa masuala ya sayansi teknolojia na ubunifu yataratibiwa vyema.

Hata hivyo Katibu mkuu huyo ameitaka Costech kuisimamia vyema miongozo hiyo kwa kuhakikisha inaleta mapinduzi makubwa katika sekta ya sayansi,teknolojia na ubunifu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa tume ya Taifa ya sayansi na teknolojia COSTECH),kupitia miongozo hiyo minne Sasa tume hiyo itasimamia vyema utekelezaji wake

"kupitia miongozo hii minne tunaanza utekelezaji wake kuanzia Leo na hapa leo hii tunafanya mdahalo hapa wa ile miongozo miwili ambayo inahusiana na mahusiano kati ya elimu ya juu,juu ya utafiti na viwanda na muongozo wa ubunifu kwa kuwa utafiti ukifanyika halafu kukawa hakuna muunganiko inakuwa ni kazi bure"amesema.

Amesema kuwa miongozo hiyo imekuja kwa wakati muafaka kwa sababu uratibu unahitajika ili kufanikisha mahitaji ya tume hiyo kwani vijana wengi wamekuja na bunifu nyingi na kusipokuwa na wa kuwasimamia huwa ni changamoto kubwa.















Post a Comment

0 Comments