WANANCHI WA MSALALA WAPONGEZA UJENZI WA BARABARA YA KAKOLA–KAHAMA




 Na mwandishi wetu

Mbunge wa Jimbo la Msalala, Mhe. Iddi Kassim Iddi, amewashukuru wananchi wa Msalala kwa uvumilivu wao wakati wa ujenzi unaoendelea wa barabara ya kutoka Kakola kwenda Kahama. Barabara hiyo, ambayo ilikuwa kilio kikubwa kwa wananchi wa Msalala kwa muda mrefu, sasa iko katika hatua za ujenzi, na matumaini ya wananchi yameanza kuonekana.


Akizungumza na Wananchi wa Kijiji Cha Bumva Kata ya Segese kuhusu maendeleo ya mradi huo, Mhe. Iddi alieleza kuwa ingawa maendeleo huja na changamoto, ni muhimu wananchi kuendelea kuwa wavumilivu kwani matokeo ya ujenzi huo yatakuwa na manufaa makubwa kwa jamii na uchumi wa eneo hilo.


"Ujenzi wa barabara hii ni hatua kubwa kwetu. Najua tumekumbana na changamoto, lakini naomba tuvumiliane. Maendeleo yanakuja na maumivu, lakini faida zake ni za muda mrefu," alisema Mhe Iddi Kassim Iddi.


Wananchi wa Msalala wamekuwa wakilalamikia hali mbaya ya barabara hiyo kwa muda mrefu, hasa kutokana na umuhimu wake kiuchumi kwa kuunganisha vijiji vya Kakola na Kahama. Ujenzi huo unatarajiwa kuleta unafuu kwa usafirishaji wa bidhaa, huduma, na watu, hivyo kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika eneo hilo.



Post a Comment

0 Comments