PAMBANO LA DULLAH MBABE NA KATOMPA LAPELEKWA ARUSHA,KUTANGAZA UTALII WA TANZANIA

 


Mkurugenzi wa Kampuni ya Lady in Red Promotion Sophia Mwakagenda akizungimza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam kuelekea pambano la Dullah Mbabe na Erick Katompa litakalofanyika Novemba 25, 2023 jijini Arusha.

NA MWANDISHI WETU

MABONDIA Dullah Mbabe wa Tanzania na Erick Katompa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo) wanatarajia kuzichapa Novemba 25 jijini Arusha.

Hayo yamebainishwa na Promota wa Pambano hilo Mkurugenzi wa Kampuni ya Lady in Red Promotion Sophia Mwakagenda akizungumza na waandishi wa habari wakati mabondia hao wakisaini mkataba kwa ajiki ya Pambano hilo.

“Leo tunekuja hapa kusainiana mkataba Kati ya Dullah Mbabe na Katompa kwa ajili ya Pambano lao litakalofanyika Novemba 25, 2023 jijini Arushu. Na lengo la Pambano hili ni kuunga mkono kuhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kukuza Utalii nchini,” amesema Mwakagenda.

Amesema kwamba Pambano hilo litakuwa la raundi 10 na litaambatana na mapambano 10 ya utangulizi.

Mwakagenda anasema Pambano hilo linakwenda na kauli mbiu ya “Boxng with Tourism” lengo likiwa ni kuutangaza Utalii, hivyo amesema anaamini Dullah Mbabe na Katompa watatimiza azima hilo la kuutangaza Utalii.

Hata hivyo amewataka mabondia wa Tanzania kutambua kuwa wanao wajibu wa kuutangaza Utalii wa nchi yao.

Kwa upande wake Bondia Dullah Mbabe amesema kwamba Pambano hilo amekuwa akilisubiri kwa hamu sana kwamba atakwenda kujiandaa vyema ili aweze kulipiza kisasi kwani Pambano lao la kwanza alipigwa.

Nao uongozi wa Chama cha Ngumi Tanzania (TPBRC) umesema kwamba utahakikisha Pambano hilo linafanikiwa. Hivyo umemhakikishia ushirikiano promota wa pambano hilo.

Post a Comment

0 Comments