TFRA yakagua shehena ya mbolea bandari kavu Dar es Salaam

 


Maafisa Udhibiti Ubora kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), John W. Sosthenes (kushoto) na Levin A Magera (katikati) wakichukua sampuli ya mbolea Amonium Sulphate eneo la Afri-ICD kabla ya kuingizwa sokoni. Kulia ni Afisa Mgomboaji (clearing and Forwarding Officer) wa kampuni ya Pamyco, Lucas Yonas akishuhudia uchukuaji wa sampuli hizo za mbolea.

Na Mwandishi Wetu 

Moja ya jukumu la Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) ni kukagua mbolea zinazozalishwa nchini au kuingizwa nchini kutoka nje ya nchi kabla ya kumfikia mkulima.

Jukumu hilo ni takwa la kisheria na linatekelezwa kikamilifu ambapo kila muingizaji wa mbolea huhakikisha mbolea yake inakaguliwa na kupewa kibali cha kuingia sokoni. 

Leo tarehe 14 Novemba, 2023 Maafisa Udhibiti Ubora kutoka TFRA, John W. Sostheness na Levin A. Magera wamefanya ukaguzi katika bandari kavu ya kampuni la Afri- ICD iliyopo eneo la Tazara, Jijini Dar Es Salaam baada ya shehena ya tani 966.28 za Mbolea ya Ammonium Sulphate (SA)21%N kuingizwa nchini na kampuni ya mbolea ya Staco Agrochem.

Katika ukaguzi huo wataalam walijiridhisha kwa kukagua nyaraka mbalimbali ikiwa ni pamoja na kibali cha kuingiza mzigo kutoka TFRA (fertilizer import permit) , Bill permit , Assesment form ya TRA na Taarifa za maabara za Mbolea kabla ya kuja nchini ili kupata taarifa za Mbolea hiyo, kabla ya kuipeleka maabara kwa uchunguzi zaidi wa kikemikali ( Chemical analysis).

Aidha, wataalam hao wamechukua sampuli kwa mjibu wa Sheria ili kupeleka maabara kujua Ubora wa Mbolea kabla haijapelekwa kwa wafanyabiashara hadi kwa mkulima. 

Utekelezaji wa jukumu hili unasaidia katika kuhakikisha wakulima wanapata mbolea bora ili waweze kuzalisha Kwa tija.


Post a Comment

0 Comments