KUPATWA KWA JUA LEO JUMATATU APRIL 08,2024

Na mwandishi wetu

MAMLAKA  ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inapenda kutoa taarifakuhusiana na 

kupatwa kwa Jua tarehe 8Aprili, 2024.

Hali ya kupatwa kwa Jua ni tukio linalohusisha kivuli cha mwezi kuangukia juu ya uso 

wa Dunia ambapo katika maeneo yaliyo ndani ya kivuli hicho Jua huonekana likifunikwa 

na Mwezi kwa kipindi cha saa chache. 

Kuna aina mbili za kupatwa kwa Jua; kupatwa kwa Jua kikamilifu ambapo mwezi 

huzuia kabisa mwanga wa Jua kufika katika Dunia na aina ya pili, kupatwa kwa Jua 

Kipete, Mwezi huzuia sehemu tu ya mwanga wa Jua, hivyo kutengeneza umbo la pete 

ya mwanga wa jua angani.

Jumatatuya Aprili 8, 2024, kunatarajiwa kutokea kwa tukio lakupatwa kwa Jua 

Kikamilifu. Tukiohililinatarajiwa kutokeaupande wa Bara laAmerika ya Kaskazini 

kupitiaMexico, Marekani na Kanada. Aidha, tukio hililinatarajiwakuanzia maeneo ya 

kusinimwa Bahari ya PasifikiambapoMexico itakuwa nchi yakwanza kufikiwa na 

kupatwa kwa Jua Kikamilifumnamo majira ya saa5:07 asubuhi kwa saaza Amerika.

Njia ya kupatwa kwa Jua itaendelea kutokeaMexico na kuingia Texas, Marekani majira 

ya saa 7:40 mchanaikipitabaadhi ya maeneona kisha kuingia Kusini mwa Ontario, 

Kanadana kutokaBara la Amerika ya Kaskazini kupitia pwani ya Bahari ya Atlantiki

katika mji waNewfoundland, Kanada, saa 11:16 jioni. 

wa kawaida, sehemu ya Jua inayofunikwa na Mwezi wakati wa kilele cha kupatwa 

kwa Jua Kikamilifuitatofautiana baina ya eneo na eneo. Maeneo yaliyo ndani ya njia ya 

kupatwa kwa JuaKikamilifuyataona kupatwa kwa Jua kwa kiwango kikubwa zaidi 

ikilinganishwa na maeneo yaliyo mbali zaidi na njia hii. 

Kwa kuwa Tanzania inaangukia katika eneo la mbali zaidi na njia hiyo, hivyo 

haitashuhudia tukio hilo.Aidha, kutokana na tukio hili kutokea mbali zaidina nchi yetu, 

athari za moja kwa moja katika masuala ya kijamii na kiuchumi hazitarajiwi kuonekana 

hapa nchini.

Mamlaka ya hali ya hewa inaendelea kufuatilia na itatoa taarifa za mabadiliko yoyote 

yanayoweza kujitokeza katika hali ya hewa kulingana na tukio hili la kupatwa kwa jua. 

Imetolewa na:

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania

Post a Comment

0 Comments