TARURA:PAIPU KALAVATI ZASAMBAZWA KURUDISHA MAWASILIANO BARABARA KILIMANJARO

 





Kilimanjaro


Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) mkoa wa Kilimanjaro wamenunua na kusambaza  paipu kalavati  kwaajili ya kurudisha mawasiliano kwenye madaraja yaliyokatika  wakati wa mafuriko kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha nchini.


Meneja wa TARURA mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Nicholas Francis amesema tayari wamepokea fedha za dharura takriban milioni 477 kwaajili ya kununua vifaa vya kukabiliana na athari za mvua.


Paipu  Kalavati ni aina ya kalavati ambazo zinaweza  kuwekwa kwa haraka pale panapotokea barabara imekatika  na hivyo huwekwa kwa urahisi na haraka ili kuweza kurudisha mawasiliano kwa wananchi na kuweza kuendelea na shughuli zao za uzalishaji.


Mhandisi Francis amesema hadi sasa paipu kalavati hizo zimeshasambazwa katika wilaya zote saba ikiwemo Same,Mwanga, Rombo,Manispaa ya Moshi,Moshi Vijijini,Hai pamoja na Siha.

Post a Comment

0 Comments