COSTECH WAZINDUA PROGRAM MBILI ZA KOMKOMBOA MWANAMKE




Na Isiaka Hamis Kikuwi

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) wamezindua program mbili Future FemTech na Kuza Tech ambazo zimelenga kumkomboa Mwanamke,Halfa ya Uzinduzi umefanyika Leo Jumanne Septemba 10,2024 Katika ofisi za Costech kijitonyama Sayansi Jijini Dar es salaam.


Akizungumza na waandishi wa Habari Mgeni Rasmi (ambaye amemwakilisha Katibu mkuu wa wizara wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia)  Mkurugenzi mkuu wa Costech Dr.Amos Nungu amesema

"programu hizi zimeundwa ili kutoa usaidizi unaolengwa kwa wajasiriamali wa kike na wasichana wa balehe, kuwapa zana muhimu, rasilimali na mitandao ili kustawi katika sekta ya teknolojia."


Future Femtech ni program ambayo umejitolea kusaidia waanzilishi wa kike katika tasnia ya teknolojia kwa kuwapa rasilimali, ushauri na ufadhili wa mbegu ili kuongeza biashara na uvumbuzi.


KuzaTech program  inalenga katika kuwawezesha wasichana wenye umri wa miaka 15-20, hasa ndani ya Dar es salaam. Programu hii ya mafunzo ya wiki 8 imeundwa ili kutoa ujuzi muhimu katika ujuzi wa kifedha, maendeleo ya biashara na uvumbuzi.



COSTECH Katika program ya Future Femtech na KuzaTech wametoa mbegu ya mfuko WA zaidi million kumi (10ml)ambazo watakabidhiwa kwa wanawake watakaofikiwa na program hizi.














Post a Comment

0 Comments