TMA YASISITIZA UMUHIMU WA MATUMIZI YA HUDUMA ZA HALI YA HEWA KWA WADAU WA UNUNUZI.

 



Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa elimu kwa wadau mbalilmbali wa Ununuzi kuhusu matumizi sahihi ya huduma za hali ya hewa pamoja na kuchangia gharama za upatikanaji wa huduma hizo katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi nchini. 

Hayo yalizungumzwa na Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Hamza Kabelwa katika mada aliyoiwasilisha katika Jukwaa la 16 la Ununuzi la Afrika Mashiriki katika Ukumbi wa AICC, Arusha, linalofanyika tarehe 09 hadi 12 Sepetemba, 2024.

Dkt. Kabelwa ameeleza kuwa, kiasi kikubwa cha matumizi ya fedha kinahusisha ununuzi, ni vyema huduma za hali ya hewa zikapewa kipaumbele katika utekelezaji wa Mipango ya Ununuzi na miradi mbalimbali ya maendeleo nchini ili kuongeza thamani ya fedha katika mradi. “Kwa kipindi cha hivi karibuni tumeshuhudia miradi mingi ikisimama kutokana na madhara yatokanayo na hali mbaya ya hewa, ni muda muafaka sasa wadau wanaohusika kuhakikisha wanatumia huduma hizo wakati wa ubunifu na kabla ya kuanza utekelezaji wa miradi yao”. Alisisitiza Dkt. Kabelwa.






Post a Comment

0 Comments