DC MAGOTI AFANYA ZIARA KIJIJI CHA KITONGA CHOLE KATA YA CHOLE

 




Na mwandishi wetu

Katika mwendelezo wa kutembelea na kufanya mikutano ya hadhara na wananchi yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. *Petro Magoti*, Octoba 09, 2024 amefanya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kitonga Chole kata ya Chole katika Wilaya ya Kisarawe.

Pamoja na Kusikiliza Kero za wananchi,Mkuu wa wilaya ya kisarawe amewataka wananchi kuacha uuzaji holela wa maeneo yao (Ardhi) kwani serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan inafanya jitihada kuhakikisha inaleta wawekezaji wengi katika wilaya ya kisarawe hususa eneo la visegese,hivyo muwe wavumilivu Ardhi yenu itapanda thamani alisema Dc Magoti.

Lakini pia,Dc Magoti amewahasa wananchi hususa vijana,kinamama na watu wenye walemavu kutumia fursa ya mikopo ya asilimia 10 za Halmashauri kwa kuunda vikundi ili waweze kupata sifa ya kuomba mikopo ya Asilimia 10% kwani Mhe. Rais Tayari ametoa utaratibu mpya na pesa tayari ipo.

Pia Dc Magoti amewahasa wananchi wa kijiji cha kitonga chole kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la uandikishaji katika daftari la kudumu la mpiga kura ili wapate fursa ya kuchagua viongozi wa serikali ya kijiji(2024) na ule wa Rais ,wabunge na madiwani mwaka 20205 zoezi hilo  litaanza octoba 11,2024.

Mwisho Dc Magoti amewahasa wananchi kua na umoja na mshikamano katika kuleta maendeleo ya kijiji na wilaya ya kisarawe kwa ujumla hususa kushiriki kujitolea katika shughuli za maendeleo ya kijamii.














#Samiamitanotena

#Kaziiendelee

#Dcmagotikazikazi

Post a Comment

0 Comments