RC CHALAMILA MTAA KWA MTAA- ILALA HAKUNA KULALA

 




Na mwandishi wetu


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila usiku wa kuamkia leo Oktoba 23,2024 amefanya ziara Wilaya ya Ilala na Kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa saa 24 pia ametembelea na kufanya mazungumzo na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Azania na Jangwani Jijini Dar es Salaam. 

Ziara ya RC Chalamila usiku wa manane inakwenda sambamba na dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ya  kufanya biashara saa 24 katika jiji la Dar es salaam ambapo Mhe Chalamila amekagua miundombinu mbalimbli ikiwemo ujenzi wa Barabara za mwendokasi BRT, uwekaji wa taa za barabarani ili kujua kama miundombinu iliyoko ni rafiki kutokana na dhamira ya Serikali ya kufanya biashara saa 24 ndani ya Jiji hilo.

"Mabasi ya Mikoani yanafanya kazi saa 24 na nchi jirani kama Kongo zinanunua bidhaa Kariakoo hivyo ni wakati muafaka kuweka mazingira ya Kibiashara katika jiji hii kufanyika saa 24 kwa masilahi mapana ya wananchi na Taifa kwa ujumla" Alisema Chalamila

Vilevile RC Chalamila akiwa katika mazungumzo na wanafunzi wa Shule ya Azania na Jangwani amewata wanafunzi kusoma kwa bidii kwa kuwa Rais Dkt Samia ameshawaboreshea mazingira ya kujisomea, pia kuchana kabisa na vitendo viovu kama kusagana na ushoga.

Sanjari na hilo RC Chalamila ameahidi kuwapatia zawadi lukuki ikiwemo mchele, ng'ombe na kutoa zawadi za mshindi wa kwanza katika mashindano ya mpira wa miguu na wa mikono kuanzia laki 2 na laki 3 kwa wavulana

Mwisho wa ziara ya usiku RC Chalamila alitembelea mradi wa ujenzi wa soko la Kariakoo lililojengwa kwa zaidi ya Bilioni 28 ghorofa kumi  ambapo mpaka sasa ujenzi umefikia asilimia 98, Soko Hilo linatarajiwa kufanya kazi masaa 24 mara baada ya kufunguliwa rasmi.




Post a Comment

0 Comments