RAIS MWINYI KUMUWAKILISHA RAIS SAMIA MKUTANO WA SADC

 






Na mwandishi wetu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi  ameondoka Zanzibar leo tarehe 19 Novemba 2024  kwenda Zimbabwe  kuhudhuria Mkutano  wa  Viongozi  Wakuu wa  nchi Wanachama wa  SADC  utakaofanyika jijini Harare.

Rais Dk, mwinyi anamwakilisha  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk, Samia Suluhu Hassan  ambae ni Mwenyekiti wa  Idara ya Siasa,Ulinzi na  Ushirikiano wa Usalama  wa  SADC.

Mkutano huo wa siku mbili utajadili  masuala mbalimbali  ya Kikanda  ikiwemo Hali ya Ulinzi na Usalama , Migogoro ya  kisiasa miongoni mwa nchi Wanachama wa SADC  ,  Tathimini ya  Matokeo ya  Uchaguzi  na hali ya kisiasa ilivyo hivi sasa nchini Msumbiji.

Post a Comment

0 Comments