Na mwandishi wetu
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Ndugu Abdulrahman A. Kassim, ameongoza kikao cha Baraza la Kikanuni UVCCM Wilaya ya Kinondoni tarehe 22 Desemba, 2024.
Awali, akifungua kikao hicho, Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Ndugu Shaweji Mkumbura, aliwapongeza Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Kinondoni kwa namna walivyoshiriki kikamilifu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2024. Pia aliwasihi kuendelea kutimiza majukumu yao kwa bidii, kwa kuzingatia kanuni za UVCCM na Katiba ya CCM.
"Nawapongeza kwa kazi nzuri mliofanya katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Endeleeni kufanya kazi kwa bidii. Mwaka 2025 tuna kazi nyingine kubwa ya kuhakikisha Daktari Samia Suluhu Hassan anapata kura za kishindo hapa Kinondoni. Umoja, mshikamano, na kufuata kanuni za UVCCM na Katiba ya CCM kutawawezesha kufanikisha haya," alisema Ndugu Shaweji Mkumbura.
Mwisho, Katibu wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Hussein Egobano, kabla ya kufunga kikao hicho, aliwasihi wajumbe wa baraza hilo kudumisha upendo na mshikamano katika utekelezaji wa majukumu yao. Alisisitiza kuepuka makundi na fitina miongoni mwao, huku akiwataka wajumbe kuiga mfano wa viongozi wao.
"Mshikamano wenu ni nguzo muhimu kwa mafanikio ya Umoja wa Vijana. Epukeni makundi na fitina, na zingatieni umoja katika utekelezaji wa majukumu yenu. Kuna watu kazi yao ni kuharibia wengine; jambo hili ni baya sana na litawakwamisha. Semeaneni mazuri na saidianeni. Mna viongozi wa wilaya wazuri; fuateni mfano wa Mwenyekiti wenu, Ndugu Abdulrahman, na Katibu wenu, Ndugu Amosi. Hawa wanashirikiana vizuri sana; sijawahi kuona wala kusikia malalamiko au shutuma baina yao," alihimiza Ndugu Hussein Egobano.
0 Comments