Lars Kare Grimsby Profesa Mshiriki Kitivo cha Mazingira na Jamii Masomo ya Kimataifa ya Mazingira na Maendeleo, Noragric kutoka Norway akizungumza na waandishi wa habari katika warsha ya nishati safi ya kupikia na mabadiliko ya tabia nchi.
NA MWANDISHI WETU
WATAFITI wa Tanzania wamekutana na watafiti kutoka Chuo cha kikuu sayansi ya maisha (NMBU) kutoka Norway wamekutana katika warsha ya Nishati safi ya kupikia na mabadiliko ya tabia nchi lengo likiwa ni kubadilishana matokeo ya tafiti ya nishati safi ya kupikia na mabadiliko ya tabia Nchi, Warsha hiyo imefanyika leo ijumaa 6 Mei 2023 katika chuo kikuu cha Dar es salaam Jijini Dar es salaam.
Warsha imeandaliwa na chuo kikuu cha Dar es salaam ambayo inalenga Kutoa ujuzi juu ya hali zinazosaidia mabadiliko ya tabia nchi na kuelekea kupikia nishati safi nchini Tanzania pamoja na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mpito wa nishati . Utafiti huo una umuhimu kwa juhudi za sasa za Dira ya Serikali ya Tanzania ya kuhamia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia na Mpango Mkakati wa utekelezaji wa Dira hiyo ambayo 80% ya watu kutumia nishati safi ya kupikia Ifakapo mwaka 2033.
Lars Kare Grimsby Profesa Mshiriki Kitivo cha Mazingira na Jamii Masomo ya Kimataifa ya Mazingira na Maendeleo kutoka Norway ambaye amewasilisha ripoti na tafiti katika warsha hiyo iliyokuwa Kumbuka Muhimu(Key Note) ya kuelewa mpito wa kupikia wa LPG wa Tanzania na Ni nini kunaweza kujifunza kutoka kwa mtazamo wa kaya na ni nini athari za hali ya Hewa ya kutoa Soma(Study) juu ya Uwezo wa Kuongezeka kwa Matumizi ya LPG kwa Kupikia katika Nchi Zinazoendelea.
Dr. Gramsby amezungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasilisha ripoti, chapisho na tafiti yake alisema"Tunataka watu wakianza kupika kwa gesi (LPG) ya kupikia badala ya kuni na kuacha kutumia umeme kwa siku za mbele inaweza cha kwanza kupunguza kiasi cha misitu ambayo inakatwa kwa ajili ya kuni na mkaa,Hivyo itapelekea kuzuia Ongezeko la joto duniani."
"kiasi cha gesi ya kupikia inaongezeka hasa miaka hii hapa ya mwishoni na imeenea, tunaona kuna kitu tunaita Energy transition kinachotokea nafikiri Tanzania na tafiti zetu inaonesha maeneo haya yanaweza kutumika kama mifano kwa watafiti wengine, kwa nchi nyingine wanapoanda sera zao za kuhamasisha watu kutumia gesi kupikia"alisema Dk. Gramsby
Ufikiaji wa Nishati kwa Wote na Upikaji safi na athari za mabadiliko ya hali ya hewa - 4CImpacts
Hivyo Ukosefu na ufikiaji wa teknolojia ya kupikia safi ndio sababu kuu ya hatari ya mazingira kwa magonjwa na ulemavu katika nchi zinazotegemea nishati asilia ya nishati ya kaya kwa sababu ya uchafuzi wa hewa wa kaya. LPG inaweza kuwa suluhisho.
Mitungi gesi (LPG) ambayo ni nashati safi ya kupikia
Nishati ya gesi ya kupikia(Liquefied PetroleumGasLPG)inatokana na malighafi ya mafuta mazito (Crude Oil)ambayo ni tafauti na gesi ya asilia ambayo inajulikana kama Liquefied Natural Gas (LNG).Lakini leo tunazungumzia chimbuko la gesi ya LPG ambayo kwa sasa ndio inatumika kwa wingi katika matumizi ya kupikia nyumbani na viwandani.
Mama akiwa anatumia nishati ya gesi katika kupikia.
Kabla kutengenezwa kuwa gesi ya LPG, nishati ya mafuta hupatikana ardhini ikiwa ni mchanganyiko wa uozo wa viumbe na mimea iliokufa kujisindika kwa miaka mamilioni yaliyopita.
Athari za 4C (4C IMPACT) ni Teknolojia, ufuatiliaji, uwekaji digitali, kujenga uwezo na ukaguzi wa mara kwa mara wa uadilifu wa Mfumo wa 4C. Leo, 4C ni mfumo unaoongoza duniani wa uidhinishaji wenye kiwango cha kina, unaojumuisha vipimo vya uendelevu wa kimazingira, kijamii na kiuchumi.
Mkurugenzi wa utafiti na machapisho Dr. Musa Mgwatu akiongea na waandishi wa habari katika warsha ya nishati safi ya kupikia na mabadiliko ya nchi.
Dk.Mussa Iddi Mgwatu ni Mkurugenzi wa Utafiti na Uchapishaji na Mhadhiri Mwandamizi wa Uhandisi Mitambo katika Idara ya Uhandisi Mitambo na Viwanda, Chuo cha Teknolojia ya Uhandisi. Maeneo yake ya utaalam ni pamoja na mifumo ya utengenezaji, uboreshaji wa mchakato, mitambo ya kiotomatiki ya viwandani, muundo unaosaidiwa na kompyuta/utengenezaji unaosaidiwa na kompyuta (CAD/CAM), na utegemezi wa mfumo uliotumika. Pia ni Mpelelezi Mkuu wa Programu Ndogo ya Usimamizi wa Utafiti wa UDSM/Sida. Dk Mgwatu alipata Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Uhandisi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Matumizi katika Uhandisi Mitambo kutoka Chuo Kikuu cha Ottawa, Kanada, na Udaktari wa Falsafa ya Uhandisi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Pia alihudhuria mafunzo ya kitaaluma kuhusu CAD/CAM katika Chuo cha Recklinghausen nchini Ujerumani.
Dk. Mgwatu alizungumza na waandishi wa habari katika warsha hiyo alisema kuwa warsha imedhamiria kubadilishana matokeo ya tafiti za nishati safi ya kupikia na mabadiliko ya tabia nchi.
Naye Joyce Msangi Afisa nishati kutoka wizara ya nishati amesema kuwa wizara ya nishati ameandaa mkakati wa miaka kumi ya utekekezaji wa Dira ya taifa ya nishati safi ya kupikia na itazinduliwa mwenzi Juni, 2023 na pia amesema tafiti hizo ni muhimu kwa kuhamasisha watu kutumia nishati safi na kuona matokeo ya tafiti hizo hivyo serikali itatumia tafiti hizo kutekeleza Dira ya kuhamia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia ifikapo 2023.
Pia warsha itakuw na mjadala wa jopo la mazungumzo (Plenary Panel discussion) ambayo watajadili Mahitaji ya maarifa na sera kwa mustakabali wa upishi safi wa Kitanzania, Mjadala utaongozwa na mwenzeshaji Dk. Remidus Ruhinduka kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam kitivo cha uchumi na kuzungumza na Ms. Joyce Msangi kutoka Wizara ya Nishati, Mr Anold Mapindunzi kutoka Baraza la Taifa la usimamizi wa mazingira Tanzania (NEMC) Eng. Finiasi Magesa chama cha nishati mpya Tanzania (TAREA) na Mr Imanuel Muro kutoka Mfuko wa Taifa mtaji wa maendeleo (UNCDP).
0 Comments